Darisalama III
(Dar es Salaam III)

kijiji changu darisalama
chenye upendo, chenye usalama
kimenilaki, kimenilea
kimekua, kimeendelea

majengo yamerefuka
watoto wamedunika
nakumisi darisalama

magari yamepaa
wadaslama wamezama
jiji limeendelea, jiji limekua

jiji la miamala
lisilona usalama
lisilona upendo
sikutaki!

~~~

Dar es Salaam III

My village Dar es Salaam
Of love and peace
accepted and nurtured me
has grown, has progressed

Buildings are rising
Children are stunting
I miss you Dar es Salaam

cars soar
Daresalamites sink
the city has progressed, the city has grown

The city full of transactions
Lacking peace
Lacking love
I hate you!

November 19, 2017

License

Poems for the Penniless Copyright © 2019 by Issa G Shivji. All Rights Reserved.

Share This Book