Ewe Ngugi wa Thiong’o
(O brother Ngugi wa Thiong’o)

Ewe ndugu Ngugi,
Wa Thiong’o.
Mwana wa Baba En’doinyo Ormoruak
Na Mama Mto Kiyiira.

Mjukuu wa Kinjikitile
Mrithi wa Ali Ponda.
Afrika ni Moja,
Vinchi ni feki.

E’nyi Waafrika,
Eti wajidai Uafrika!
Ndoto zenu Kireno,
Lugha yenu Kimarekani.

Walimu wenu wafadhili,
Eti wahisani.
Viongozi wenu mafisadi,
Eti wa-utandawazi.

Amkeni, Waafrika.
Uafrika ni Umajumui wa Afrika.
Oteni ndoto, Kizaramo,
Fikra, Kiswahili; mawazo Kigikuyu.

Fuateni nasaha za Sheikh Ali bin Ponda:
‘Baba ni Afrika, Mama ni Afrika’.
Silaha ni U-africa,
Askari ni Afrika Moja.

Nkosi sikelele Afrika.
Mungu ibariki Afrika.

~~~

O brother Ngugi wa Thiong’o

O brother Ngugi,
Wa Thiong’o.
Son of En’doinyo Ormoruak, the father
And Mto Kiyiira, the mother.

Grandchild of Kinjekitile
Successor of Ali Ponda.
Africa is one
Statelets are fake.

O you Africans
Pretending Africanness!
You dream in Portuguese,
And speak American.

Your teachers are donors,
Supposedly benefactors.
Your leaders are corrupt,
Supposedly globalized.

Wake up Africans.
Africanness is Pan-Africanism.
Dream in Zaramo,
Think in Swahili, ponder in Gikuyu.

Listen to Sheikh Ali bin Ponda:
‘Father is Africa, Mother is Africa.’
The weapon is Pan-Africa,
The soldier is One Africa,

Nkosi sikelele Africa.
God bless Africa.

August 11, 2009

License

Poems for the Penniless Copyright © 2019 by Issa G Shivji. All Rights Reserved.

Share This Book