Kamaradi Ndimara
Umerejea ukamaradi
Nakupongeza kwa dhati.

Defeat au victory, isikusumbue,
Wajibu wetu ni kuendelea
Kupambana.

Wenye njaa sio wachoyo,
Wao, hujitolea,
Hutoa mwanga,
Mwanga wa Ukombozi.

Leo, kesho, na milele,
Usemi wa Mao hauna ubishi.
“Wherever there is oppression,
there is bound to be resistance”.

Swali sio kusherehekea,
Au kunung’unika.
Swali ni, unasherehekea nini?
Na unasherehekea na nani?

Wako wenyenchi,
na wananchi.
Ingawa, tunahubiriwa,
Umoja, utulivu, na amani.
Nani wametulia?
Umoja wa tabaka? Tabaka lipi?
Kuna amani na Amani,
Amani huyu ni nani?

Analinda amani ya akina-nani?
Umoja wa tabaka gani?

Ndimara, ndugu yangu,
Labda tumepitwa na wakati,
Lakini, Historia sio muda au wakati,
Historia ni mapambano,
Mapamabano yanaendelea,
Historia inakua.

Ni Historia ya wanyonge,
Wanaandika kwa damu.
Wakipepea bendera,
Bendera Nyekundu.

Wako katika Mapambano,
Na Ukombozi.

~~~

Congratulations Comrade Ndiimara

Comrade Ndimara[1]
To comradeship, you have returned
For that, my hearty congratulations.

Let not defeat or victory torment you,
Our duty is the continuation
Of the struggle.

The hungry are not greedy,
They are giving,
They give light,
Light of liberation.

Today, tomorrow and forever,
Mao’s saying is unarguably correct.
“Wherever there is oppression,
there is bound to be resistance”.

The issue is not of celebrating,
Or of moaning.
The issue is, what is one celebrating?
And with whom is one celebrating?

There are those who own the country,
And those who belong to the country.
Although, we get preached upon,
Unity, tranquility and peace.
Who is patient?
Class alliance? Which class?
There is peace and Peace,
Who is he, this Peace?

Whose peace is being secured?
Unity of which class?

Ndimara my brother,
Maybe the times have passed us by,
But, History is not a period or time,
History is struggles,
The struggle continues,
History moves.

It is the History of the weak,
Who write with their blood.
While waving the flag,
That red flag.

Yours in the Struggle
for liberation.

Issa Bin Mariam, 2003


  1. This was written to Ndimara Tegambwage, one of the leading journalists in Tanzania. He was one of the founders of the movement for the restoration of multiparty politics in Tanzania; and served as member of parliament for one term. The original poem was written to welcome him back to his profession

License

Poems for the Penniless Copyright © 2019 by Issa G Shivji. All Rights Reserved.

Share This Book