Lugha ya ukimya
(Language of silence)

Kuna ukimya na ukimya
Kuna ukimya wa busara
Kuna ukimya wa kutia hasara
Kuna ukimya wa uoga
Kuna ukimya wa kupanga
Kuna ukimya wa hofu
Kuna ukimya wa kutarajia dafu
Kuna ukimya wa mkakati
Kuna ukimya wa wakati

Kupanga ni kuchagua
Kuropoka ni kujiponza

Kuna lugha na lugha
Lugha ya kutusi
Lugha ya kusifu
Lugha ya kupendeza
Lugha ya kujipendekeza
Lugha ya kuimba
Lugha ya kuvinda
Lugha ya kuchambua
Lugha ya kutumbua
Lugha ya kifumbo
Lugha ya kitumbo
Lugha ya kufarajisha
Lugha ya kutisha

Mfumbo unakufikirisha
Tumbo linakudhalalisha

~~~

Language of silence

There is silence and silence
There is the silence of wisdom
There is the silence that results in loss
There is the silence of fear
There is the panned silence of planning
There is the silence of fear
There is the silence waiting for a break
There is the silence of the strategy
There is the timely silence

Planning is choosing
Blabbing is jeopardising

There is language and language
Insulting language
Praise language
Beautiful language
ingratiating language
Singing language
Hunter’s language
Criticising language
Disemboweling language
Metaphorical language
Accumulating language
Refreshing language
Scary language

Riddles make you think
The stomach humiliates you

January 9, 2019

License

Poems for the Penniless Copyright © 2019 by Issa G Shivji. All Rights Reserved.

Share This Book