Mwaka mpya I
(New Year I)

ninachukua nafasi hii
bila kupewa
ninatumia kisingizio cha mwaka mpya
bila kuficha
kuwatakia kila la heri
maisha mema yenye afia na maadili
maisha ya mapambano
mapambano ya kujenga
jamii bora
jamii yenye haki
jamii yasiyo na dhulma
jamii ya usawa, ubinadamu na utu
Alamsiki

~~~

 

 

New Year I

Though not sought to
I dare take this opportunity
With the new year as my pretext
Without reservation
I wish you all the best
Good life full of good health and righteous conduct
A life full of struggles
Of positive struggles
For a better society
A just society
Non-oppressive society
A society that is equal, empathic and humane
Goodnight

December 24, 2017

License

Poems for the Penniless Copyright © 2019 by Issa G Shivji. All Rights Reserved.

Share This Book