Issa amechokonoa nyuki
Waliofungiwa mzingani
Wakila asali masegani
Naye mrina keshawasili
Moto keshaukoka kondeni
Apate kuirina asali

Kama ilivyo jana na juzi
Walipojikuta matatani
Wakichuma nta mauani
Hawakujichanganya kundini
Walienda wawili wawili
Wakapuliziwa sumu moshi
Na kugaragara ardhini
Waliporejea mzingani
Haraka wakazitafakari
Harakati nayo mikakati
Vilingeni na barabarani
Wakaamua na kumaizi
Kusambaratika ni rahisi
Muwapo ni wawiliwawili
Peke muvamie harakati
Kiwango cha umma wa jumui.
Ila umekwishakumaizi?
Mgawanyiko wa mzingani
Vibarua mbali na walinzi
Mijadala mbali na ukuli
Unakumbuka kazimzumbwi
Na wanaTanga hivi majuzi
Nani wanafanya tafakuri?
Mrina akiwapo kondeni
Yako wapi makundi ya nyuki
Yajipenyeze nje ya moshi
Yajiunge na siafu kufuni
Zivunjwe tabaka mzingani
Nazo za wasomi na watendi!

~~~

Response from Demere Kitunga

Issa has disrupted the bees
Enclosed colony in the hive
Feasting in the honeycombs
And the harvester has arrived
The fire is ready in the field
Harvesting is to go ahead

Just like yesterday and the day before
When they found themselves in trouble
When gathering pollen from the flowers
Detached from the group
They went two by two
Got poison smoke sprayed upon
And rolled over on the ground
Back in the hive
Quick they had to envision
The struggle and its strategies
On stage and open roads
They made decisions and realized
Disintegration is easy
When in pairs
Only invade the struggle
At leves of communal masses.
But have you understood?
The division at the hive
Workers apart from guards
Debates apart from labour
You remember the Kazimzumbwi saga?
And people of Tanga just recently?
Who is analysing?
With the harvester in the field
Where are the bee colonies?
To pierce through the smoke
Join hands with the bonded ants
To break the classes in the hive
Those of scholars and doers!

January 2007

License

Poems for the Penniless Copyright © 2019 by Issa G Shivji. All Rights Reserved.

Share This Book