Salamu za asubuhi
(Good morning)

nawasalimu kwa tabasamu
tabasamu za matumaini
kwa neno la wahenga
lililosheheni busara za kale
hekima za leo
mwongozo wa siku zijazo

wahenga husema
hata mawingu manono
yana cheche za radi
yakilipuka yanaunguza
yakitulia yanaangaza

~~~

Good morning

I greet you with smiles
smiles of hope
with a word of wisdom
from the sages
insights from today
guidelines for tomorrow

sages say
even heavy clouds
have sparks of thunder
that burn when exploding
shine when calm

January 5, 2018

License

Poems for the Penniless Copyright © 2019 by Issa G Shivji. All Rights Reserved.

Share This Book